SPORTS

 

Unknown Unknown Author
Title: SANE AKARIBIA KUJIUNGA NA MANCHESTER CITY.
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Leroy Sane anakaribia kumaliza uhamisho wake katika klabu ya Manchester City kutoka Schalke kwa kitita cha pauni milioni 37. Klabu hiyo...
Leroy Sane anakaribia kumaliza uhamisho wake katika klabu ya Manchester City kutoka Schalke kwa kitita cha pauni milioni 37.
Klabu hiyo ya Bundesliga ilitangaza siku ya Jumatatu kwamba kiungo huyo wa kati hakujiunga nao wakati wa mazoezi yao huko Austria kabla ya kuanza kwa msimu ujao na kwamba alisalia Manchester.
Mkufunzi wa klabu ya Man City Pep Guardiola alithibitisha mnamo tarehe 21 mwezi Julai kwamba alitaka kumsajili Sane.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 20 aliisaidia Ujerumani kufika nusu fainali za Euro2016, baada ya kucheza mechi yake ya kwanza ya kimataifa mnamo mwezi Novemba.
Alimwambia mkurugenzi wa michezo katika klabu hiyo Christian Heidel kwamba alitaka kuondoka katika klabu hiyo.









About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top