
Kamati ya kimataifa ya OLimpiki IOC
imetangaza kuwa inaunda jopo la wanachama watatu ambao watatoa uamuzi wa mwisho
wa wanariadha wageni wa Urusi watakaoshiriki mashindano ya olimpiki ya Rio De
Jenairo huko nchini Brazil ambayo yanatarajiwa kuanza Ijumaa hii.
Msemaji wa kamati hiyo Mark Adams,
ameuambia mkutano wa waandishi wa habari kuwa jopo hilo litatathmini kesi
zinazowakumba wanariadha wote wa Urusi.
Jopo hilo la maafisa watatu linawajumuisha
Ugur Erdener, raisi wa mchezo wa mishale , Claudia Bokel ambaye anahudumu
katika jopo la Wanariadha la kamati ya Olimpiki IOC na mwakilishi wa
Uhispania Juan Antonio Samaranch ,
Kufikia sasa wanariadha 250 wa Urusi
walikuwa wameruhusiwa kushiriki mashindano hayo ya Olimpiki ya Rio.
Shirika la kupambana na matumizi ya
madawa ya kuongeza nguvu mwilini WADA lilikuwa limependekeza wanariadha wote
kutoka Urusi wapigwe marufuku ya Kushiriki michezo yote ya kimataifa kufuatia
ufichuzi uliobainisha kuwa serikali ya Urusi ilihusika katika njama ya kuficha
matumizi ya madawa ya kuongeza nguvu miongoni mwa wanamichezo wake.
Post a Comment