
Kipa nambari moja wa
klabu ya Manchester United David De gea amesema ujio wa nyota wa Sweden Zlatan
Ibrahimovic imeongeza hamasa ya hali ya juu kikosini hapo.
Ibrahimovic 34, alipewa
jezi yenye namba 9 mgongoni alipofika baada ya kukamilisha dili la usajili huru
toka klabu ya PSG ya nchini Ufaransa kuja kuungana na aliyewahi kuwa kocha wake
wa zamani Jose Morinho.
Morinho pia amewanunua,
beki wa Ivory Coast Eric Bailly na raia wa Armenia Henrikh Mkhitaryan na De Gea
amekubali uwezo wa wachezaji wote kwa muda mchache ambao wamekuwa kwenye
mazoezi pamoja.
‘‘Ni jambo zuri sana kuwa na Zlatana hapa tayari, akifanya mazoezi na
timu, unaweza kuona ni mchezaji mzuri, akiwa shupavu na sifa zote za kuwa
mshambuliaji tayari anazo” De Gea aliiambia MUTV.
‘‘Nafikiri ataendana na mazingira kwa haraka Zaidi, unaweza kuona na
anaoneka kama alikuwa anacheza hapa kwa muda mrefu sasa na sawa kwa wachezaji
wengine ambao wote tumejumuika nao” Alisema De Gea.
‘‘Wanacheza vizuri sana mazoezi yao yamekuwa ni ya hali ya juu sana na
naweza kusema ya kuwa tumesajili watu sahihi ambao wanatupa nguvu, unapoona
wachezaji kama wao wanakuja hapa Manchester na sasa tumewajaribu wote kwa
pamoja, kujaribu kuwaweka sawa kwa upesi zaidi na sasa tunakwenda kucheza mechi
kubwa mechi ya ngao ya hisani dhidi ya mabingwa Leicester city”
Post a Comment