
Klabu ya wekundu wa Msimbazi Simba, wameendelea na michezo ya
kirafiki huko mjini Morogoro, ambapo jana tena walikuwa uwanjani na
kuwashuhudia wakitoka kifua mbele baada ya kuwafunga klabu ya Burkinafaso kwa
ushindi mujarabu wa magoli 5-0
Magoli ya Simba yaliwekwa kimyani na mshambuluaji wao machachari
Ibrahimu Ajibu aliyepachika magoli mawili wakati Ndusha akifunga goli moja, na
Shiza Kichuya aliyesajiliwa kutoka Mtibwa Sugar naye akafungua hazina ya magoli
wakati lile la mwisho likipachikwa nyavuni na Said Ndemla.
Tangu wameweka kambi jijini Morogoro, klabu ya Simba
imekwisha cheza mechi 3 akiwa ameshinda zote wakati ile ya awali ilikuwa ni
dhidi ya Polisi Morogoro walipowabugiza magoli 6-0 wakati mchezo mwingine
ulikuwa dhidi ya Moro Kids waliposhinda goli 2-0 na wakitarajiwa kucheza mchezo
mwingine dhidi ya timu ya Manispaa ya Kinondoni na ndipo watarudi jijini Dar
kwaajili ya kujiandaa na Simba Day watakapokuwa na mchezo wa kirafiki dhidi ya
klabu ya kutoka Angola Inter-crop.
Post a Comment