Kocha huyu anachukua nafasi iliyoachwa na Gerardo
"Tata" Martino aliyejiuzulu baada ya kumalizika kwa michuano ya kombe
la Copa America walipokubali kipigo cha mikwaju ya penalty dhidi ya Chile
AFA walimtangaza kocha huyo baada ya klabu ya Sao Paulo
kukubali kumuachia kocha huyo kwenda kukinoa kikosi cha timu ya taifa ya
Argentina.
Bauza, mwenye umri wa miaka 58, alikua kocha mkuu wa
klabu ya Sau Paulo toka mwaka 2015 na kuisaidia kufika nusu fainali ya michuano
ya Copa Libertadores, hivyo ataiongoza Argentina katika kampeni za kusaka
tiketi ya kombe la dunia la 2018 bila ya staa wa taifa hilo Lionel Messi
aliyejiuzulu baada ya kumalizika kwa Copa America.
Makocha waliokua wakipewa nafasi ya kukinoa kikosi hicho
ni Jorge Sampaoli Marcelo Bielsa pamoja na Diego Simeon na Mauricio Pochettino.
Post a Comment