SPORTS

 

Unknown Unknown Author
Title: ubelgiji yatupwa nje ya mashindano.
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Wales wajihakikishia nafasi ya kusonga mbele.   Na Charles Kunji. Michuano ya Euro hatua ya robo fainali imendelea tena kwa m...
Wales wajihakikishia nafasi ya kusonga mbele.
 


Na Charles Kunji.


Michuano ya Euro hatua ya robo fainali imendelea tena kwa mchezo wa pili ambapo timu ya taifa ya Wales imeichabanga vvilivyo timu ya taifa ya Ubelgiji kwa jumla ya magoli 3-1.
Alikuwa ni Radja Nainggolan dakika ya 13 alipowasimamisha Mashabiki wa ubelgiji baada ya kuukwamisha mpira wavuni na kuiandikia timu yake goli la uongozi kabla ya Ashley kurudisha goli dakika ya 31 na kuufanya ubao usomeke 1-1 mpaka kipindi cha kwanza kinamalizika.
Kipindi cha pili kilianza kwa mashmabulizi ya kushtukiza kwa kila timu lakini ilipofika dakika ya 55 Hal Robson-Kanu akaipatia Wales goli la pili kabla ya Sam Vokes kumalizia mpira kwa kichwa safi dakika ya 86 na mpaka mwamuzi anapuliza filimbi kumaliza mpira, tayari Wales pamoja na mashabiki wao walikuwa wamesimama kuishangilia furaha waliyokuwa nayo.


Kwa mara ya mwisho timu ya wales kushinda katika mashindano makubwa kama haya ilikuwa ni mwaka 1958, na mwaka huu wamefuzu wakiwa chini ya kocha wao Chris Coleman  mpaka wanafika nusu fainali kucheza na timu ya taifa ya Ureno walioifunga Poland kwa mikwaju ya penalty 5-4. Baada ya kuushuhudia mchezo wao kwenda dakika 120 wakiwa wamefungana 1-1
Siri kubwa ya timu ya Wales ni kuwa na mshambuliaji anayekipiga katika klabu ya Real Madrid Gareth Bale na Aron Ramsey ambao wameweza kuiongoza timu kucheza kwa umoja na kufika hapa walipofika.

Michuano hiyo itaendelea tena siku ya kesho ambapo timu ya taifa ya ujerumani itawavaa timu ya taifa ya italia katika hatua ya robo fainali ya tatu kabla ya mechi ya mwisho katika hatua ya robo fainali ambapo wenyeji wa michuano hiyo ufaransa watakipiga na timu ya taifa ya Iceland.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top