SPORTS

 

Unknown Unknown Author
Title: MARTINEZ ATEULIWA KUWA KOCHA WA UBELGIJI.
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Meneja wa zamani wa vilabu vya Everton, Wigan na Swansea, Roberto Martinez ameteuliwa kuwa mkufunzi mkuu wa timu ya taifa ya Ubelgi...
Roberto Martinez



Meneja wa zamani wa vilabu vya Everton, Wigan na Swansea, Roberto Martinez ameteuliwa kuwa mkufunzi mkuu wa timu ya taifa ya Ubelgiji.

Martinez, 43, ambaye ni raia wa Uhispania, alifutwa kazi Everton mwezi Mei baada ya kufanya kazi Goodison Park kwa miaka mitatu.

Marc Wilmots alijiuzulu wadhifa wake kama meneja wa Ubelgiji mwezi jana, wiki mbili baada ya yakukubali kipigo dhidi ya Wales robo fainali katika michuano ya Euro 2016.

Nafasi yake ilitangazwa wazi mtandaoni na Shirikisho la Soka la Ubelgiji.
Shirikisho hilo lilisema linamtafuta mtu bingwa katika mawasiliano na mwenye uwazi na ambaye amethibitisha uzoefu katika kuwapa wachezaji nyota ujuzi na ustadi katika ufundi.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top