SPORTS

 

Unknown Unknown Author
Title: GABRIEL JESUS KUCHEZA ETIHAD KWA MIAKA MITANO.
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Siku chache baada ya matajiri wa jiji la Manchester, klabu ya manchester city kukamilisha dili la usajili wa mjerumani Leroy Sane tok...


Siku chache baada ya matajiri wa jiji la Manchester, klabu ya manchester city kukamilisha dili la usajili wa mjerumani Leroy Sane toka klabu ya Shakle 04 ya Ujerumani, klabu hiyo tena imefanikiwa kumpa kandarasi ya miaka 5 mchezaji kinda toka nchini brazil, Gabriel Jesus kwa kitita cha pauni milion 27 akitokea klabu ya Palmeiras.

Man city wamempa Jesus mkataba huo wa miaka mitano lakini ataendelea kubaki katika klabu ya Palmeiras mpaka mwisho wa msimu wa ligi ya Brazil na atajumuika na kikosi cha matajiri hayo mnamo mwezi december mwaka huu.

Jesus alichaguliwa kama mchezaji bora chipukiziwakati akiwa Palmeiras na kiifungia klabu hiyo magoli 26 katika mechi 67 alizocheza na hadi sasa akiwa kama mfungaji bora katika ligi hiyo.

Man city wameipiku Barcelona waliokuwa wanataka kumsajili kinda huyo anayetarajiwa kuoingoza timu yake ya taifa ya Brazil katika mashindano ya Olimpic yanayofanyika mchini humo.


Mpaka sasa matajiri hao wametumia karibu ya pauni milion 100 kwa kuwasajili wachezaji kama vile Norito, Gundogan Sane pamoja na kinda huyo wa brazili Gabriel Jesus.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top