SPORTS

 

Unknown Unknown Author
Title: RUNGU LA CAF LAIPATA TIMU YA WANAWAKE YA EQUATORIAL GUINEA.
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Timu ya taifa ya Equetorial Guinea ya wanawake, imefungiwa kushiriki katika fainali za kombe la mataifa ya Africa kwa upande wa wanawake ...
Equatorial Guinea are out of 2020 Olympics qualifying
Timu ya taifa ya Equetorial Guinea ya wanawake, imefungiwa kushiriki katika fainali za kombe la mataifa ya Africa kwa upande wa wanawake katika fainali tatu mfululizo kwa kumtumia mchezaji ambae hakustahili kucheza.
Mwezi Agosti, shirikisho la mpira la dunia FIFA, lilibaini kuwa mchezaji Camila Maria do Carmo Nobre de Oliveira alikuwa anamiliki paspoti mbili za kusafiria na vyeti viwili vya kuzaliwa vyenye tarehe tofauti, na kufuatia hayo, wakawa wametolewa katika hatua za mwanzoni za kufuzu michezo ya Olympic za mwaka 2020.
Shirikisho la mpira barani Africa, CAF limewaadhibu tena taifa hilo la Equetorial Guinea kwa kosa hilo hilo.
Kupitia mtandao rasmi wa shirikisho hilo, viongozi wa CUF wamesema hayo yamefanyika baada ya taifa la Mali kupinga matokeo ya Equetorial Guinea kushinda goli 3-2 yao katika raundi ya mwisho ya kufuzu fainali za kombe la mataifa.
Camila Nobre do Carmo Oliviera alipangwa kwenye mechi dhidi ya mali, michezo iliyofanyika tarehe 6 na 10 ya mwezi April. Kufuatia uchunguzi wa CUF ulibaini ya kuwa mchezaji huyo alikuwa amesajiliwa kwa jina la Camila Maria Nobre Carmo katika fainali za AFCON kwa wanawake za mwaka 2014 zilizofanyika huko Namibia huku tarehe yake ya kuzaliwa ikiwa ni 7/10/1994 na kwa mashindano yam waka huu, cheti chake cha kuzaliwa kikiwa kinasomeka kama alizaliwa tarehe 10/6/1988 huku kikiwa na jina la Camila Nobre do Carmo Oliviera".

Shirikisho la mpira chini humo limekiri kuwa tatizo hilo limeweza kujirudia, Camila Nobre do Carmo Oliviera ameweza kufungiwa miaka mitatu lakini pia na taifa kwa upande wa timu ya wanawake wakati nafasi ya E Guinea itachukuliwa sasa na timu ya taifa ya Mali katika michuano hiyo itakayofanyika nchini Cameroon kuanzia November 19  mpaka December 3.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top