SPORTS

 

Unknown Unknown Author
Title: DE BRUYNE ASISITIZA GUARDIOLA KUPEWA MUDA ZAIDI.
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Mchezaji wa kimataifa wa klabu ya Manchester City na timu ya taifa ya Ubelgiji Kevin De Bruyne amesisitiza kwamba kocha wa klabu hi...



Mchezaji wa kimataifa wa klabu ya Manchester City na timu ya taifa ya Ubelgiji Kevin De Bruyne amesisitiza kwamba kocha wa klabu hiyo raia wa Hispania Pep Guardiola atachukua muda mrefu kuleta falsafa na mbinu zake katika klabu hiyo ya jijini Manchester.

De Bruyne, 25 ni moja ya wachezaji wa klabu ya Manchester City walioitwa katika timu za taifa kwenye mashindano ya EURO ya mwaka huu na mashindano ya Copa America, ni yeye pekee aliyerejea katika mapumziko yao ya muda mrefu na kujiunga na timu hiyo katika mazoezi ya Alhamisi

 ‘‘Amebadilisha baadhi ya vitu vichache klbu hapa” Alisema De Bruyne alipokuwa akihojiwa na kituo cha TV cha skysports.

‘‘Bila shaka ndio itamchukua muda kidogo haswa kwa wale ambao wamechelewa kujiunga na kikosi hicho. Ni vigumu sana kujenga timu wakati watu wengine wakija nje ya muda baada ya EURO pamoja na Copa America”

Kocha Guardiola raia wa Hispania aliacha kazi ya kuifundish klabu ya Bayern Munich na kuingia mkataba wa kukinoa klabu hicho cha Manchester City akichukua nafasi ya Manuel Pelegrin aliyetimuliwa.

Matajiri hao wa jijini Manchester wataanza kampeni yao ya kulisaka kombe la EPL kwa mchezo dhidi ya klabu ya Sunderland katika uwanja wao wa Etihad siku ya tarehe 13 mwezi huu.



About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top