
Meneja wa Liverpool Jurgen Klopp amesema mshambuliaji Mwitaliano Mario
Balotelli anafaa kutafuta klabu mpya.
Balotelli, 25, alikuwa katika klabu ya AC Milan ya nchini Italy kwa
mkopo msimu uliopita lakini amerejea Liverpool kwa mazoezi ya kabla ya msimu.
Mchezaji huyo wa zamani wa Manchester City amefungia Liverpool
mabao manne tangu ajiunge na klabu ya Liverpool msimu wa 2014.
“Hayumo katika kiwango cha uchezaji ambapo anafaa kuwa
akishindania nafasi moja au mbili na wachezaji wanne au watano,” amesema Klopp.
“Kwa hivyo, ni wazi kwamba tunahitaji suluhu. Kutakuwa na klabu
ambayo itakuwa na furaha kuwa na Mario Balotelli mpya." Alimalizia Klopp.
Baloteli aliyekuwa na msimu mzuri akiwa na klabu ya Manchester City
na kufanya vyema, anatarajiwa kujiunga na klabu yeyote itkayaonyesha kumhitaji
mwitaliano huyo.
Post a Comment