SPORTS

 

Unknown Unknown Author
Title: Sam Allardyce: akubali mazungumzo na FA.
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
  Klabu ya Sunderland imekubali viongozi wa FA kufanya mazungumzo na kocha wao juu ya kuingia mkataba wa kukinoa kikosi cha taifa ya E...

 Embedded

Klabu ya Sunderland imekubali viongozi wa FA kufanya mazungumzo na kocha wao juu ya kuingia mkataba wa kukinoa kikosi cha taifa ya England.
Lakini klabu ya Sunderland inayoshiriki ligi ya EPL imesisitiza ya kuwa bado inamhitaji Allardyce kwani yeye ni mtu muhimu sana klabuni hapo. Allardyce aliweza kuinusuru klabu hiyo kushuka daraja msimu uliomalizika kwa kumaliza msimu wakiwa wa 17 katika msimamo mbele ya Aston villa, News castle pamoja na Norwich timu zote zikiwa zimeshuka daraja.
FA wanahaha kupata saini ya kocha mwingine baada ya aliyekuwa kocha wa England, Roy Hogson kujiuzulu baada ya timu yake kutolewa katika hatua ya mtoano [16 bora] na timu ya taifa ya Iceland kwa magoli 2-1
Sam Allardyce aliye na timu huko nchini Austria kwa maandalizi ya msimu ujao, anatarajiwa kurudi nchini Wingereza wiki moja kabla ya kuanza rasmi kwa msimu wa 2016-2017, unaotarajiwa kuanza rasmi juma la pili la mwezi agosti.
Sunderland wamekubali, japo kwa shingo upande kwa kujua vyema ile ndio silaha yao, na wamependekeza endapo kutakuwa hakuna maelewano, basi wasiweze kurefusha mazungumzo.
                                            

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top