Aliyewahi kuwa mwandishi wa BBC. auawa Burundi.
Bi Hafsa Mossi, Aliyewahi kuwa
mtangazaji wa michezo na habari nyingine katika Shirika la Habari la BBC
kupitia Idhaa ya Kiswahili, Hafsa Mossi ameuwawa kwa kupigwa risasi.
Hafsa ambaye alikuwa Mbunge wa Bunge
la Afrika Mashariki kutoka Burundi Hafsa Mossi ameuawa na watu wasiojulikana
mjini Bujumbura, leo.
Mtandao wa BBC umesema Hafsa
aliyekuwa wakati mmoja Waziri wa Masuala ya Afrika Mashariki katika serikali ya
nchi hiyo, aliuawa kwa kupigwa risasi katika barabara ya Gihosha, eneo la
Nyankoni.
Msemaji wa rais wa Burundi, Willy
Nyamitwe amesema amesikitishwa sana na mauaji ya mwanasiasa huyo.
“Nimesikitishwa
sana. Dadangu mkubwa Hafsa Mossi, mwanachama wa @EA_Bunge amefariki, amepigwa
risasi na wahalifu. R.I.P #Burundi,” ameandika kwenye Twitter.
I'm shocked. My
elder Sister Hafsa Mossi Member of the @EA_Bunge
has passed away, shot by criminals. R.I.P #Burundi
Waziri wa mambo ya nje Alain Aime Nyamitwe pia
ameeleza kusikitishwa kwake na mauaji hayo.
“Nimehuzunishwa sana na mauaji ya leo#Bujumburaya
Mheshimiwa Hafsa Mossi, na mwanachama wa#EALA. Ni hasara kuu kwa taifa na#EAC,”
ameandika kwenye Twitter.
Post a Comment