
Na mwandishi wetu, Charles Kombe.
Matajiri wa jiji la
Manchester, Klabu ya Manchester City wamemsajili mchezaji kutoka
Colombia, Marlos Moreno kwa kitita cha paun milioni 4.75 kwa
kandarasi ya miaka mitano.
Kinda huyo mwenye umri wa
miaka 19 atakwenda klabu ya Uhispania Deportivo La Coruna kwa mkopo
msimu wa 2016/17.
Marlos Moreno anakuwa
mchezaji wa tatu kusainiwa na Pep Guardiola katika wiki hii, baada ya
kuwasili kwa winga Leroy Sane kutoka clab ya Schalke 04 pamoja na
kinda wa Brazil Gabriel Jesus Kutoka klabu ya Palmeiras ya nchini
Brazil.
Tangu Mhispania huyo
achukue nafasi ya Manuel Pellegrini kama meneja mwezi julai,
Guardiola ametumia kiasi cha £100m hadi kufikia sasa.
Moreno aliandika katika
wavuti ya clab hiyo kuwa “ "Pep Guardiola ni moja ya mameneja
bora duniani. Nadhani anapenda wachezaji chipukizi zaidi na anaweza
kuwafunza zaidi wachezaji chipukizi kwa mbinu pamoja na ufundi,
Itakuwa jambo kubwa sana kufanya kazi naye na kua miongoni mwa timu
kubwa” alisema Moreno.
Hata hivyo katika
kuimarisha kikosi chake, Bosi huyo wa zamani wa Bayern Munich na
Barcelona Pep Guardiola amelipa kipaumbele swala la kuwasajili
wachezaji chipukizi watakao kuwa ghali zaidi katika kipindi kijacho.
Muispania huyo pia ana
ndoto za kumsajili beki wa Everton na timu ya taifa ya England Johns,
ambapo clab hiyo ya England imetangaza kutaka paun mil.50 kwa timu
itakayomsajili beki huyo.
Post a Comment