SPORTS

 

Unknown Unknown Author
Title: KLOPP AIADHIRI BARCELONA.
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Katika mwendelezo wa mechi za kirafiki zinazoendelea, mchezo kati ya klabu ya Liverpool na Barcelona umeweza kumalizika kwa Klabu ya ...


Katika mwendelezo wa mechi za kirafiki zinazoendelea, mchezo kati ya klabu ya Liverpool na Barcelona umeweza kumalizika kwa Klabu ya Barcelona kukubali kufungwa goli 4-0 dhidi ya klabu ya Liverpool iliyo chini ya mwlimu Jugen Klopp, raia wa Ujerumani.

Ushindi mujarabu wa Liverpool ulifunguliwa dakika ya 15, ambapo mchezaji ingizo jipya aliyesajiliwa toka klabu ya Southampton Sadio Mane alipoukwamisha mpira wavuni, kabla ya Mascherano kujifunga wakati Divock Orig na Grucij wakikamilisha idadi hiyo ya magoli manne.

Mabingwa hao wa ligi ya Hispania, klabu ya Barcelona walipanga kikosi chote isipokuwa yule mchezaji wao muhimu Neymer ambae analitumikia taifa lake katika mashindano ya Olympic yanayoendelea huko Rio nchini Brazil.


Klopp amesema japo wameshinda, lakini bado hawako vizuri sana nab ado ana kazi ya kukitengeneza kikosi hicho ili kiwe kikosi cha ushindani na hadhi ya klabu hiyo iweze kurejea kama zamani.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top