picha na salehe jembe. |
WAZIRI
wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye, amesema tayari
wameshakamilisha mfumo wa utumiaji wa tiketi za elektroniki kwenye Uwanja wa
Taifa jijini Dar, na muda wowote zitaanza kutumika.
Ni kwa muda mrefu serikali
ilitangaza kuweka mfumo wa tiketi hizo kwenye viwanja inavyovimiliki vya Uhuru
na Taifa, lakini suala hilo lilionekana kama kusuasua kabla ya hivi karibuni
kutiliwa mkazo na hatimaye kukamilika.
Awali ilielezwa kuwa, Jumapili iliyopita
ndiyo serikali itakabidhiwa mfumo huo baada ya kukamilika, lakini zoezi hilo
likaahirishwa kutokana na shughuli za kiserikali kuingiliana.
“Kila kitu kimekamilika na
nimehakikishiwa hilo na wale tuliowapa kazi hiyo, ile ratiba ya awali ya
kukabidhiana nimeiahirisha mimi na si mwingine kwa sababu siku tuliyopanga
awali mimi nilikuwa Dodoma kwenye shughuli nyingine za kiserikali.” Nape
alisema.
Nape alisisitiza kuwa, wikiendi hii
ndiyo wanatarajia kulifanya zoezi hilo la makabidhiano.
Post a Comment