SPORTS

 

Unknown Unknown Author
Title: SEMINA ELEKEZI KWA AJILI YA SOKA LA WANAWAKE.
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
SHIRIKISHO la mpira wa miguu nchini TFF, limeanda semina elekezi kwa klabu za Ligi Kuu za wanawake ikiwa ni sehemu ya maandalizi ...




SHIRIKISHO la mpira wa miguu nchini TFF, limeanda semina elekezi kwa klabu za Ligi Kuu za wanawake ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya ligi hiyo inayotarajia kuanza rasmi mapema mwezi ujao. 

Semina hiyo iliyokuwa ifanyike siku ya jumamosi, inaendelea sasa hivi kwenye Ukumbi wa Hosteli za TFF zilizopo ofisi za Makao Makuu ya shirikisho hilo Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume ulioko makutano ya barabara za Shaurimoyo na Uhuru jijini Dar es Salaam.

Ligi hiyo ya wanawake ni ya kwanza kufanyika nchini chini ya uongozi wa Rais Jamal Malinzi kwani kabla ya hapo hapakuwa na ligi inayohusisha mikoa mbalimbali. Shukrani za pekee ziende kwa Kituo cha Televisheni cha Azam, kilichoamua kudhamini ligi hiyo pamoja na ile ya vijana wenye umri wa chini ya miaka 20.

TFF imeandaa semina hiyo kwa ajili ya kuwapa maelekezo kuhusu kanuni za ligi, usajili wa timu na taratibu nyingine za ligi hiyo ikiwa ni pamoja na sheria za mpira wa miguu ambazo zimekuwa na marekebisho kwa msimu wa 2016/2017 kama zilivyotolewa na Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA).

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top