
KLABU
ya Yanga imeendelea kunyimwa pointi katika uwanja wa Nangwanda Sijaona uliopo
Mjini Mtwara baada ya hapo jana kulazimishwa sare tasa ya bila kufungana dhidi
ya trimu ya Ndanda FC.
Katika mechi tano
walizokutana kati ya klabu ya Yanga na Ndanda, sare zimezidi kutawala ambapo
kuna sare 3 huku Yanga wakishinda mchezo 1 kama walivyofanya Ndanda katika
mchezo wa kwanza wa timu hizi tangu Ndanda apande daraja.
Ndanda
ikiwa inacheza mchezo wake wa kwanza kwenye uwanja wa nyumbani iliweza kuhimili
mashambulizi ya Yanga ambayo pia ilikuwa ikicheza mchezo wake wa kwanza ugenini
tangu kuanza kwa ligi msimu wa 2016-2017.
Licha
ya kufanya mashambulizi ya mara kwa mara, wachezaji wa Yanga walishindwa kupata
goli na kujikuta wakipata kona nyingi kutokana na walinzi wa Ndanda kuokoa
mashambulizi ya hatari yaliyofanywa na Yanga.
Post a Comment