SPORTS

 

Unknown Unknown Author
Title: FIFA YALETA WARAKA MPYA WA USAJILI.
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
SHIRIKISHO la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA), limesambaza waraka mpya kwa wanachama wake, likiwamo Shirikisho la Mpira wa Miguu ...


Image result for fifa world cup images

SHIRIKISHO la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA), limesambaza waraka mpya kwa wanachama wake, likiwamo Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) ukisema mameneja wote wa usajili wa wachezaji kwa mfumo wa Mtandao (TMS-Transfer Matching System Managers) hawana budi kujiunga na mawasiliano mapya ili kupata taarifa mbalimbali za usajili na uhamisho wa wachezaji.

FIFA limeleta mfumo huo unaoitwa GPX yaani Global Players Exchange ambao malengo yake ni kurahisisha kufanya usajili kwa mchezaji mmoja kwenda timu nyingine lakini kabla ya kufanya hivyo utasaidia kupata taarifa kamili za mchezaji huyo na shabaha kuu ni kurahisisha mawasiliano ya TMS Managers nchi nzima, klabu na mashirikisho mbalimbali duniani.

Hiyo inakuja baada ya baadhi ya mashirikisho kama vile TFF kuwa na matatizo lukuki ifikapo kipindi cha usajili na hivyo itasaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza matatizo yafananayo na hayo.






About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top