
MSIMU mpya wa ligi kuu ya England umefunguliwa rasmi hapo
jana baada ya kushuhudia timu kadhaa zikichuana kwa ajili ya kupata pointi tatu
muhimu katika michezo yao ya awali.

Leo hii kutakuwa na mchezo mkali wa kusisimua ambapo, washika
mitutu wa London, Arsena, watakuwa na kibarua watakapokuwa wanawakaribisha
Liverpool, mchezo utakaofanyika saa 18:00 kwa majira ya Afric mashariki.
Klabu ya Arsenal yenye makazi yake Kaskazini mwa jiji la
London, chini ya mkufunzi wao Arsene Wenger, anatarajiwa kuanzisha majeshi yake
yote, huku akiwa na nafasi kubwa ya kumwanzisha mchezaji wao mpys Granit Xhaka,
raia wa Uswis.

Kwa upande wa Juggen Klopp, akiwa anachagizwa na ushindi wa
goli 4-0 dhidi ya mabingwa wa ligi ya Hispania, klabu ya Barcelona katika
mchezo wa kirafiki, anatarajiwa kuwa na kikosi ambacho kinaweza kuwa na sura
ngeni haswa usajili wa Sadio Mane wa pauni 30mil kutoka klabu ya Sauthampton
baada ya kuonyesha mchango mkubwa kwenye kikosi hicho wakati wa mechi za
kirafiki.
Aidha, kwa mechi kumi zilizopita, Klabu ya Liverpool
wanaonekana kutokuwa na matokeo mazuri kwani wameshinda mechi moja pekee huku
akilazimisha sare mechi nne na kufungwa mechi tano.
Timu. GP
W D L
Arsenal 10 5
4 1
Liverpool. 10 1
4 6
Mchezo wa mwisho wa January mwaka huu, katika uwanja wa
Anfield, waliweza kutoka sare ya goli 3-3, ikiwa ni sare yenye magoli mengi tangu
mwaka 2009 walipotoka sare ya goli 4-4.
Arsenal haijawahi kufungwa na Liverpool katika uwanja wa
Emirates tangu mwaka 2012, wakati tangu mwaka 2010, mchezo kati ya vilabu hivi,
umetoa kadi nyekundu 5, 3 zikiwa kwa upande wa Liverpool wakati 2 zikienda kwa
klabu ya Arsenal.
Leo klabu ya Liverpool watajitupa tena uwanjani wakiwa hawana
rekodi nzuri mbele ya klabu ya Arsenal, Washika mitutu wa jiji la London,
Dakika 90 za mwamuzi ndizo zitakazoamua ni nani ataibuka kidedea kuelekea
mchezo huo
karata yangu mimi ni kwa Klopp, hata ukiangalia uswajili alioufanya, na mentality ya timu nzima hakika watakuwa na msimu bora
ReplyDelete