SPORTS

 

Unknown Unknown Author
Title: WAKIMATAIFA BHANA, SASA WANAKUMBUKA SHUKA WAKATI KUMEKUCHA.
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
MCHEZO wa raundi ya tano wa kombe la shirikisho barani Africa uliopigwa jijini Dar es salaam, umemalizika kwa klabu ya Yanga kuibuka...
IMG_0004



MCHEZO wa raundi ya tano wa kombe la shirikisho barani Africa uliopigwa jijini Dar es salaam, umemalizika kwa klabu ya Yanga kuibuka na ushindi wa goli 1-0 dhidi ya klabu ya MO Bejaia ya nchini Algeria.

Tambwe ndie aliyepachika bao hilo la ushindi akimalizia mpira wa faulo uliopigwa na Thaban Kamusoko dakika ya pili ya kipindi cha kwanza. Ushindi huo bado hauwezi kuisogeza popote klabu ya Yanga, kwani bado itaendelea kuburuza mkia huku akiwa na pointi nne pekee, nyuma ya Mo Bejaia na Medeama walio na pointi tano wote kwa pamoja huku Mazembe akiwa kinara wa kundi hilo akiwa na pointi 10 kibindoni.

Japo nafasi ya klabu ya yanga ni finyu mno, bado wana nafasi ya kusonga mbele endapo watashinda mchezo wao wa mwisho dhidi ya timu ya TP Mazembe ya nchini Congo.

Hizi ni hesabu tu ambazo wakati mwingine huwa hazina nafasi sana katika mchezo wa soka kwani wakati unataka kupata matokeo Fulani, huku unakuwa unmwombea mpinzani wako mabaya, kiukweli ni hesabu ambazo huwa hazina kichwa wala miguu.


Kikubwa ambacho kipo kwa sasa ni kukubali ya kuwa Yanga walichelewa sana, kama wangepata matokeo katika michezo ya awali, hakika leo angekuwa anachekelea, sasa badala yake, huu mchezo unabaki kama kukamilisha ratiba lakini pia wao kuonyesha ya kuwa walikuwa wamekata tamaa,waliuita ni mchezo wa kirafiki.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top