
MSAMBULIAJI nguli wa klabu ya Barcelon na timu ya taifa ya Argentina, Lionel
Messi amethibitisha nia yake ya kurejea timu ya taifa kwa mujibu wa kauli aliyoitoa
jana usiku.
Nyota huyo wa Barcelona alifanya uamizi wa kustaafu soka la
kimataifa baada ya kupoteza mchezo wao wa fainali ya Copa America dhidi ya
Chile mwaka 2016.
Baada ya kufanya mazungumzo na kocha mpya wa Argentina
Edgardo Bauza, Messi amefikia uamuzi wa kurejea tena kwenye timu ya taifa.
“Naona
kuna matatizo mengi kwenye soka la Argentina na nisingependa kuona
yanaongezeka,” amesema leo.
“Sitaki
kuleta maafa, siku zote nimekuwa nikijitahidi kufanya kila niwezalo kuisaidia
timu.
“Tunapaswa
kutatua mambo mengi sana katika soka la Argentina, lakini natakiwa kufanya hilo
nikiwa ndani ya timu na sio kukosoa nikiwa nje.”
“Wakati
wa fainali ile, nilikuwa na msongo wa mambo mengi sana kichwani mwangu na
kikukweli niliamua kuachana na timu ya taifa, lakini mapenzi yangu kwa nchi hii
na hii jezi yamenifanya nirudi,” amesema.
“Nadhani
watu wote ambao wanataka mimi kuendelea kuwaepo kwenye timu ya taifa, natumaini
sasa tutafurahia pamoja.”
Post a Comment