SPORTS

 

Unknown Unknown Author
Title: HII SI YA KUKOSA, KLOPP VS WENGER.
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
MSIMU mpya wa ligi kuu ya England umefunguliwa rasmi hapo jana baada ya kushuhudia timu kadhaa zikichuana kwa ajili ya kupata pointi...


MSIMU mpya wa ligi kuu ya England umefunguliwa rasmi hapo jana baada ya kushuhudia timu kadhaa zikichuana kwa ajili ya kupata pointi tatu muhimu katika michezo yao ya awali.
Leo hii kutakuwa na mchezo mkali wa kusisimua ambapo, washika mitutu wa London, Arsena, watakuwa na kibarua watakapokuwa wanawakaribisha Liverpool, mchezo utakaofanyika saa 18:00 kwa majira ya Afric mashariki.

Klabu ya Arsenal yenye makazi yake Kaskazini mwa jiji la London, chini ya mkufunzi wao Arsene Wenger, anatarajiwa kuanzisha majeshi yake yote, huku akiwa na nafasi kubwa ya kumwanzisha mchezaji wao mpys Granit Xhaka, raia wa Uswis.
Photo published for ‘You must live with what you missed’


Kwa upande wa Juggen Klopp, akiwa anachagizwa na ushindi wa goli 4-0 dhidi ya mabingwa wa ligi ya Hispania, klabu ya Barcelona katika mchezo wa kirafiki, anatarajiwa kuwa na kikosi ambacho kinaweza kuwa na sura ngeni haswa usajili wa Sadio Mane wa pauni 30mil kutoka klabu ya Sauthampton baada ya kuonyesha mchango mkubwa kwenye kikosi hicho wakati wa mechi za kirafiki.

Aidha, kwa mechi kumi zilizopita, Klabu ya Liverpool wanaonekana kutokuwa na matokeo mazuri kwani wameshinda mechi moja pekee huku akilazimisha sare mechi nne na kufungwa mechi tano.
Timu.                            GP   W   D   L    
Arsenal                          10   5   4   1
Liverpool.                       10   1   4   6

Mchezo wa mwisho wa January mwaka huu, katika uwanja wa Anfield, waliweza kutoka sare ya goli 3-3, ikiwa ni sare yenye magoli mengi tangu mwaka 2009 walipotoka sare ya goli 4-4.

Arsenal haijawahi kufungwa na Liverpool katika uwanja wa Emirates tangu mwaka 2012, wakati tangu mwaka 2010, mchezo kati ya vilabu hivi, umetoa kadi nyekundu 5, 3 zikiwa kwa upande wa Liverpool wakati 2 zikienda kwa klabu ya Arsenal.


Leo klabu ya Liverpool watajitupa tena uwanjani wakiwa hawana rekodi nzuri mbele ya klabu ya Arsenal, Washika mitutu wa jiji la London, Dakika 90 za mwamuzi ndizo zitakazoamua ni nani ataibuka kidedea kuelekea mchezo huo

About Author

Advertisement

Post a Comment

  1. karata yangu mimi ni kwa Klopp, hata ukiangalia uswajili alioufanya, na mentality ya timu nzima hakika watakuwa na msimu bora

    ReplyDelete

 
Top