
KLABU ya Simba imepokea kwa
mshtuko mkubwa taarifa ya msiba wa watoto wa mchezaji wetu Juuko Murshid
vilivyotokea leo huko kwao nchini Uganda.
Vifo vya watoto hao watatu vimekuja katika kipindi hiki ambapo
mchezaji wetu huyo wa kimataifa, akiwa kwenye maandalizi ya fainali za
mashindano ya Afcon, yanayotarajia kuanza katikati ya mwezi ujao.
Tunajua uzito wa kufiwa na watoto hao, na tunatambua uchungu
alionao nyota wetu huyo, yeye pamoja na mkewe, lakini tunaamini Mungu atawapa
subira na uvumilivu mkubwa katika kipindi hiki kigumu wanachopitia.
Mwisho klabu inawatakia Wanasimba na Watanzania wote heri ya
mwaka mpya 2017.
Imetolewa na.
*Haji S Manara*
Mkuu wa Habari wa Simba SC.
Post a Comment