
BAADA ya kuonyesha kiwango
cha juu kwenye mechi ya kufunga mwaka dhidi ya Middlesbrough, kocha wa
Manchester United, Jose Mourinho, amesisitiza ya kuwa Martial asimsikilize
wakala wake na badala yake amsikilize nini anachokisema yeye.
Martial jana aliiongoza United kupata ushindi
wa 2-1 na kusogea mpaka kuwa na pointi 36 huku Martial akifunga moja ya magoli
hayo.

Martial, 21, alisajiliwa mwaka 2015 akitokea
Monaco na kuwa mfungaji bora wa msimu uliopita kwenye timu ya Manchester United
akiiubka na magoli 17.
Wakala
wa Martial amekuwa akifanya mazungumzo na mabingwa wa kombe la EUROPA, sevilla
juu ya Martial kujiunga nayo.
Lakini tangu amekuwa akipewa nafasi na
Mourinho, Martial amekuwa akifanya vizuri kiasi cha kumshawishi abatilishe
maamuzi yake.
Post a Comment