
MABINGWA watetezi wa ligi kuu ya
England, Leicester City wamekamilisha dili la kumsajili mchezaji wa KRC Genk,
Wilfred Ndidi.
Ndidi,
20, raia wa Nigeria amesaini kandarasi ya miaka mitano na nusu ya kuitumikia
klabu ya Leicester.
Mchezaji
huyo anatarajia kuja kuziba pengo la Kante ambaye alitimkia Chelsea Julay ya mwaka
jana.
Ndidi
ameisaidia Genk kufuzu kwenye
hatua ya 32 ya EUROPA huku akiisaidia timu yake kwenye ligi ya Ubelgiji.
Mambo
mengine juu ya mkataba wake watawekwa hadharani baada ya kumaliza vipimo vya
afya atakavyokuwanavyo kwenye wiki hii kama ilivyoripotiwa na mtandao rasmi wa
klabu.
Post a Comment