SPORTS

 

Unknown Unknown Author
Title: WACHEZAJI WA TIMU YA TAIFA YA WANAWAKE YA NIGERIA WAONDOKA HOTELINI BAADA YA KUPEWA STAHIKI ZAO.
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
TIMU ya wanawake ya Nigeria imesitisha mgomo wao wa kukaa hotelini baada ya kulipwa stahiki zao walizokuwa wameahidiwa. Timu hiyo i...
Nigeria celebrate winning the Women's Africa Cup of Nations

TIMU ya wanawake ya Nigeria imesitisha mgomo wao wa kukaa hotelini baada ya kulipwa stahiki zao walizokuwa wameahidiwa.

Timu hiyo ilikuwa inalidai shirikisho la mpira la nchi hiyo NFF kiasi cha US$23,650  kwa kila mchezaji baada ya kutwaa ubingwa wa timu za wanawake kwa bara la Africa.

Wadada hao wanaojulikana kwa jina la The Super Falcon, wamekuwa hotelini katikati ya jiji la Abuja tangu tarehe 6 ya mwezi December yam waka huu.

"Wachezaji wameshaondoka wote hapa hotelini baada ya kupokea stahiki zao walizokuwa wameahidia na NFF” Ofisa habari wa timu hiyo Remi Sulola alikiambia kituo cha bbc.

Moja ya wachezaji hao pamoja na mwenzake wa chumba walichokuwepo wamethibitisha kupokea fedha hizo.

"Inaweza ikachukua muda hivi kwa sababu mabenki mengi hayafanyi kazi siku za wikiendi, lakini hatimaye tumekwisha pokea kilicho chetu” Alisisitiza dada mmoja ambaye hata hivyo aliomba kuhifadhiwa jina lake.

"Tunaishukuru serikali, mashabiki pamoja na vyombo vya habari ambao mlitusaidia kuhakikisha tunapata haki zetu”


About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top