SPORTS

 

Unknown Unknown Author
Title: MZAMIRU, MO WAIREJESHA SIMBA KILELENI.
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
TIMU ya Ndanda FC ya mjini Mtwara imeendeleza uteja mbele ya timu ya Simba baada ya kukubali kichapo cha goli 2-0 kwenye mchezo uliofa...
img_4382



TIMU ya Ndanda FC ya mjini Mtwara imeendeleza uteja mbele ya timu ya Simba baada ya kukubali kichapo cha goli 2-0 kwenye mchezo uliofanyika katika dimba la Nangwanda Sijaona, mjini Mtwara.

Alikuwa ni Mzamiru Yassini na Mohamed Ibrahim, MO waliopachika mabao hayo na kuirejesha Simba kileleni kwa jummla ya pointi 38 huku wakiwaacha mahasimu wao kwa wao Yanga kwa pointi mbili baada ya kukaa kileleni kwa muda.

Tangu klabu ya Ndanda ipande daraja msimu wa mwaka 2014, haijawahi kupata matokeo yoyote chanya mbele ya wekundu wa msimabazi Simba.

Takwimu Simba vs Ndanda tangu mwaka 2014.
18/12/2016 Ndanda FC 0-2 Simba
20/08/2016 Simba 3-1 Ndanda FC
10/03/2016 Simba 3-0 Ndanda FC
01/01/2016 Ndanda FC 0-1 Simba
25/04/2015 Simba 3-0 Ndanda FC
17 01/2015 Ndanda FC 0-2 Simba.
Matokeo mengine ni:
Mbao FC 1-0 Stand United
African Lyon 0-0 Azam FC
Tanzania Prisons 1-0 Majimaji FC



About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top