BAADA ya mshambuliaji wa kimataifa wa klabu ya Azam
kuafikiana na timu hiyo, mshambuliaji huyo raia wa Ghana, Samuel Afful, ameanza
kupiga mkwara ya kuwa timu yao itakuwa bora msimu ujao kutokana na watu waliosajiliwa
kwenye timu hiyo.
Afful, aliyetokea klabu ya Sekondi Hasaacas ya huko Ghana,
amejitia kitanzi cha miaka mitatu cha kuitumikia klabu hiyo huku akiungana na
wenzake Waghana waliosajiliwa na Azam FC msimu huu, beki wa kati Daniel Amoah,
winga Daniel Atta Agyei na mshambuliaji Yahaya Mohammed.
Uwezo wake ulianza kuonekana pale alipofunga goli moja katika
mechi ya kirafiki dhidi ya Ruvu Shootimg, pale Azam walipoibuka na ushindi wa
goli 3-1.
Akizungumza na mtandao rasmi wa klabu
ya Azam FC www.azamfc.co.tz Afful amesema
kwa aina ya wachezaji waliosajiliwa tokea Ghana akiwemo na yeye, basi ni
dhahiri kuwa Azam itakuwa na safu bora ya ushambuliaji.
“Nimefurahishwa sana kujiunga na Azam
FC kama mchezaji mwingine anavyofurahia kusaini mkataba mpya, namshukurtu Mungu
kwani yeye ndiye aliyefanikisha hili, nimejiandaa vilivyo kuisaidia timu hii na
naamini kwa namna nilivyowaona wachezaji kwenye mechi mbili walizocheza na
usajili uliofanywa Azam FC itakuwa moto kwa mechi zinazokuja na eneo la
ushambuliaji litakuwa tishio” Alisema Afful,
Post a Comment