
KOCHA
msaidizi wa timu ya Simba, Jackson Mayanja amesema wao wanachoangalia ni
kusonga mbele ili kutimiza adhma yao ya kumaliza ligi raundi ya kwanza wakiwa
kifua mbele ili kurejesha furaha kwa mashabiki wa timu hiyo ambao wameikosa kwa
muda mrefu.
Mayanja ameyazungumza hayo tokea jijini Mbeya
ambapo baadae, watakuwa na mechi dhidi ya maafande wa jeshi la magereza,
Tanzania Prisons ili kusaka pointi tatu muhimu.
Hata hivyo, timu zote zitaingia uwanjani zikiwa na
kumbukumbu ya kupoteza michezo yao ya mwisho ambapo, Simba walipoteza dhidi ya
African Lyon, ikiwa ndio mechi yao ya kwanza kufungwa tangu msimu umeanza huku
Prisons wakifungwa na mabingwa watetezi Yanga.
“Sisi
tunaangalia mbele hatuangalii nyuma, tunataka kuona tunapata ushindi kwenye
mechi ya mwisho ya mzunguko wa kwanza ili tubaki kwenye nasafi ya kwanza kwenye
ligi.”
“Mashabiki wasikate tama waendelee kuishangilia
timu yao Simba ni timu yao wasikate tama kwa kupoteza mchezo huu.”
“Mwaka huu tunaomba Mungu tuweze kufikia malengo ya
wanachama kwasababu wanachama wanamuda mrefu hawajaona kombe.”
Mechi nyingine itakuwa katika dimba la Mwadui
Complex ambapo wenyeji, Mwadui FC watawakaribisha
Post a Comment