
HII inakuwa ni mara ya kwanza kwa Pep Guardiola akiwa kama kocha kuifundisha timu na ikacheza bila kupata ushindi kwa mechi 6 mfululizo.
Wakati mwingine sio jambo jema sana kwani hata baadhi ya vyombo vya habari vya Hispania kuazna kudodosa ya kuwa uwepo wa Guardiola Mancity na staa wa timu hiyo, raia wa Argentina, Sergio Aguero.
Mambo yalianza kwenda mrama baada ya Mancity kulazimishwa sare ya bao 3-3 dhidi ya Celtic kwenye kombe la Klabu bingwa la Ulaya.
Baada ya hapo Guardiola akakumbana na kibano kingine toka kwa klabu ya Tottenham cha goli 2-0 kwenye ligi kuu ya England.
Licha ya kufanya mabadiliko ya hapa na pale kwenye kikosi, bado mambo yaliendelea kuwa si shwari kwani mado kuna matokeo mengine ya ligi pamoja na Efl.
MECHI ZOTE 6 DHIDI YA MANCITY.
Celtic 3-3 Mancty.
Tottenham 2-0 Mancty.
Everton 1-1 Mancty.
Barcelona 4-0 Mancity
Southampton 1-1 Mancity.
MaUnited 1-0 Mancity.
Baada ya matokeo yasioyoridhisha, kocha Guardiola atakuwa anaiongoza timu yake ya Mancty kuikabili West Brom, je ataendeleza rekodi hiyo?
Post a Comment