
MCHEZAJI wa zamani wa klabu
ya Manchester United na Mancity, Carlos Teves amejiunga rasmi na timu ya
Shanghai ya nchini China.
Teves, 32 aliyekuwa
anakipika katika klabu ya Boca Juniors, amejiumga na Shanhgai licha ya mkataba
wake kutokuwekwa wazi na timu hiyo.
Shanghai, waliowahi kufundishwa na kocha wa
zamani wa klabu ya Brighton, Gus Poyet, aimeripoti kukubaliana na Teves kwa
dili la £40m huku akitarajiwa kulipwa £310,000 kwa wiki.
Uongozi wa Boca Junior umemtakia maisha mema
huko Teves aendako na kuongeza kuwa bado wanaheshimu mchango wake klabuni.
Tevez amecheza kwa misimu 7 katika ligi ya EPL
na kushinda mataji kwa pande zote za Manchester.
Teves pia alifanikiwa kutwaa kombe la UEFA
mwaka 2008 akiwa na Manchester United kabla hajaihamia Juve mwaka 2013 ambako
pia alitwaa Serie A mara mbili.
Post a Comment