
MENEJA wa kikosi cha Mbeya
City, Godfrey Katepa amesema tayari Mbeya City wamejifua vyema kuwakabili Toto
Africans ya jijini Mwanza kwenye mchezo namba 130 wa VPL utakaopigwa kwenye
dimba la kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya hapo kesho.
Akizungumza na mtandao rasmi wa
Mbeyacityfc.com Katepa amesema, “Hali ya kikosi chetu ni nzuri kabisa, hakuna
mchezaji yoyote aliye majeruhi, Haruna shamte aliyekuwa na maumivu ya kifundo
cha mguu amerejea kikosi baada ya matibabu ya siku kadhaa jopo la madaktari
wetu wametuthibitishia kuwa yuko sawa tayari kwa mchezo wa kesho, ni wazi
hakuna kinachotuzuia kushinda mchezo huo” Katepa alisema.
Aidha, akizungumzia suala la Ngassa, Meneja
amethibitisha ya kuwa hatokuwepo kwenye mchezo wa kesho kutokana na baadhi ya
mambo kutokukamilika.
“Ni wazi ataukosa mchezo
huu, suala lake bado halijakamilika, jambo muhimu ni kuwa uongozi bado
unaendelea kufanya mawasiliano na klabu ya Fanja kuhakikisha
linakamilika ili aweze kuichezea timu yake mpya kwenye michezo ijayo, awali
walitutumia TPO pekee, hivyo tunasubiri RELEASE LETTER kutoka kwao ili
tuweze kupata ITC kwa mujibu wa taratibu, ilikuwa watutumia jana
lakini mtu ambaye alipaswa kufanya hiyo kazi alikuwa nje ya Oman na
anarejea leo.
Hatuna msuguano wowote na Fanja
kama inavyoripotiwa mawasialino kati yetu ni mazuri kama ilivyo kwa Tff na
chama cha mpira cha Oman hivyo siku si nyingi suala hili litafikia
mwisho alimaliza”
Mechi nyingine.
LEO;
African Lyon vs Yanga,
KESHO;
Mwadui vs Mbao FC.
Ndanda RC vs Mtibwa Sugar
Kagera Sugar vs Stand United.
Majimaji FC vs Azam FC
Post a Comment