
CLAUDIO Ranieri amekosoa
adhabu aliyopewa mshambuliaji wake Jamy Vardy ya kadi nyekundu na kukosa mechi
tatu.
Leicester
walikata rufaa ya adhabu hiyo ambayo hata hivyo rufaa yenyewe ilitupiliwa mbali
na shirikisho la mpira wa miguu la England, FA.
Vardy,
ambaye ni mfungaji bora wa Leicester msimu uliopita, alionyeshwa kadi nyekundu
kwenye mechi dhidi ya Stoke na adhabu yake inaanza kuhesabiwa kwenye mechi ya
jumatatu dhidi ya Everton.
"Kila
mmoja hapa England na duniani kote alitazama mechi na kukubali ya kuwa ile wala
haikuwa faulo ya kiasi hicho” Alisema Ranieri.
"Tulikata
rufaa kwa sababu tulikuwa tunaamini ya kuwa tutapata haki yetu lakini tumekuwa
disappointed kwa matokeo ya rufaa yetu na hii inamaanisha ya kuwa hata
wachezaji wakifanya makosa basi sisi tusikate rufaa kwa sababu rufaa zetu huwa
zinakatiwa” Aliongeza Ranieri.
Kuelekea
mchezo boxing day, siku ya jumatatu, mabeki, Christian Fuchs na Robert Huth,
nao pia watakuwa wakitumikia adhabu kwenye mechi ya Everton huku Midifilda,
Danny Drinkwater yupo mashakani kama atacheza au laa kutokana na kusumbuliwa na
kifundo cha mguu.
"Hata
hivyo, hii itakuwa ni nafasi kwa wachezaji ambao huwa hawapati nafasi kwenye
kikosi cha kwanza na kunishawishi ili niendelee kuwatumia kwenye michezo
mingine.
Post a Comment