
Oscar ambaye amekuwa akihaha kupata namba ya kuanza
kwenye kikosi cha Conte, anatarajia kuungana na bosi wake wa zamani, Andre
Villas-Boas huko Shanghai.
Hata upande wa Shanghai, nao pia wameshathibisha ya
kuwa Oscar atajiunga nao muda si mrefu kwenda kuwaongezea nguvu.

Thamani ya uhamisho wa Oscar inatarajiwa kuingia
kwenye rekodi za dunia ya kuwa atakuwa mmchezaji wa saba kununuliwa ghali zaidi
duniani na atakuwa analipwa kiasi cha paundi 400,000 kila wiki.
Dirisha la usajili linatarajiwa kufunguliwa siku ya
mwaka mpya na kufungwa tarehe 23 ya mwezi
January.
Usajili wa Oscar
unakuja siku chache baada ya uvumi wa nyota wa zamani wa timu ya Manchester
City, Carlos Teves kujiunga na ligi ya China na kukadiriwa kuwa na mshahara
mnono zaidi duniani.
Post a Comment