SPORTS

 

Unknown Unknown Author
Title: MATIC AMPIGIA CHEPEO BATSHUAYI KWA CONTE.
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
MCHEZAJI wa Chelsea, Nemanja Matic amesema, Michy Batshuayi endapo atapewa nafasi kwenye mchezo wa boxing day dhidi ya Bournemouth, ...


MCHEZAJI wa Chelsea, Nemanja Matic amesema, Michy Batshuayi endapo atapewa nafasi kwenye mchezo wa boxing day dhidi ya Bournemouth, huenda akampora namba mshambuaji wa kutegemewa wa timu hiyo, Diego Costa.

Costa, ambaye ni top-scorer kwenye EPL kwa sasa, ataokosa mchezo huo baada ya kuonyeshwa kadi tano za njano na Batshuayi aliyejiunga na Chelsea akitokea Olympique de Marseille amekuwa akihusishwa kuwa chaguo la Conte kwenye mchezo wa Boxing day.

"Unapokuwa na Costa kwenye timu yako na anacheza vizuri na kuscore magoli, ni vigumu sana kupata namba mbele yake kama ni mzima na hana majeraha, lakini naamini Micky anaweza kwani anajituma sana” Alisema Matic.

Batshuayi ameshinda mara tatu kwenye michezo 13 aliyocheza Chelsea, na Matic anaamini Micky ndiye mchezaji pekee wa kumrithi Costa.

"Bila shaka amekuwa anamfaidi sana Costa na kujifunza vingi kutoka kwake, Ni sawa na mimi miaka saba iliyopita, nilikuwa nafurahi na kujifunza vingi toka kwa Frank Lampard, Michael Ballack na Michael Essien jinsi walivyokuwa wanacheza” Aliongeza Matic.

"Hivyo, ni vizuri kwa micky kutokana na kupata uzoefu toka kwa Costa na faida kubwa ikiwa ni kwamba huku bado ana nafasi ya kucheza nae.”


Kwenye mchezo huo, Kante pia atakuwa nje kwa kosa kama la Costa na hivyo Fabregas akitarajia kuungana na Matic kwenye idara ya kiungo siku watakapowakaribisha Bournamouth.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top