SPORTS

 

Unknown Unknown Author
Title: KRC GENK YAITAMBIA KAA GENT BILA YA KOCHA WAO PETER MAES.
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
TIMU ya KRC Genk leo ilikuwa katika dimba la Luminus Arena kuwakaribisha mahasimu wao KAA Gent bila ya aliyekuwa kocha wao Peter Maes ...




TIMU ya KRC Genk leo ilikuwa katika dimba la Luminus Arena kuwakaribisha mahasimu wao KAA Gent bila ya aliyekuwa kocha wao Peter Maes na kuibuka na ushindi wa goli 2-0.

Magoli ya Genk yamewekwa kimiani Aljandro Pozuelo dakika ya 19 ya mchezo na Nikolas Karelis, aliyefunga kwa mkwaju wa penalty dakika ya 25.

Genk waliokuwa wakicheza chini ya mkufunzi msaidizi wa zamani wa klabu ya Manchester United, Albert Stuivenberg bado wameendelea kusalia kwenye nafasi ya 9 huku wakiwa na pointi 28 wakati vinara wa ligi hiyo, Club Brugge wakiwa na pointi 43 lakini wakiwa wamecheza mechi moja Zaidi ya Genk.


Nahodha wa timu ya taifa ya Tanzania, Mbwana Samatta aliingia dakika ya 51 akichukua nafasi ys Kaleris.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top