
BAADA
ya kukaa kwa muda mrefu asijue nini kinachoendelea, Faridi Muussa sasa anataria
kuondoka nchini kuelekea Hispania ili kujiunga na klabu ya Tenerife ya ligi
daraja la kwanza, [Segunda Devision]
Afisa habari wa klabu ya
Azam FC amelithibitisha hilo kwa kuonyesha tiketi atakayoitumia Faridi kwenye
safari yake ya kesho.

“Kama mtakumbuka tuliwaambia Farid Musa taratibu zake zinakwenda vizuri,
aliitwa ubalozini akapeleka passport yake na mkataba wake na Azam FC.
Ninapoongea na ninyi ni kwamba, klabu ya Tenerife ya Spain imetuma tiketi ya ya
Farid Musa ambapo anatarajiwa kuondoka tarehe 28 (kesho) kuelekea Spain
kujiunga na klabu yake,” anasema Jafar Idd wakati akizungumza na waandishi wa
habari.
Post a Comment