SPORTS

 

Unknown Unknown Author
Title: FURAHA YA HAZARD NI KUENDELEA KUWEKA REKODI NDANI YA CHELSEA.
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
HUU ndio msimu bora sana kwa klabu ya Chelsea walio chini Antonio Conte, baada ya kuendeleza rekodi yao ya kutokupoteza mchezo kwenye l...




HUU ndio msimu bora sana kwa klabu ya Chelsea walio chini Antonio Conte, baada ya kuendeleza rekodi yao ya kutokupoteza mchezo kwenye ligi kuu ya EPL.

Ushindi wa jana wa Chelsea wa 3-0 dhidi ya FC Bournamouth ulikuwa ni ushindi wa 12 mfululizo kwa timu hiyo kushinda.

 Lakini kikubwa Zaidi ni ule mwendelezo wa wachezaji kuendelea kujiwekea rekodi zao ndani ya klabu ya Chelsea.

Eden Hazard jana alifanikiwa kufunga bao moja na kufikisha idadi ya magoli 50 na akiingia kwenye rekodi ya watu 6 waliowahi kufunga mabao Zaidi ya 50.

Baadhi ya wachezaji wa Chelsea waliowahi kufunga magoli Zaidi ya 50 ni Lampard, Drogba, Hasselbaink, Zola na Gudjohnsen.


Hatimaye Hazard ameingia kwenye kundi hili na anaonekana kuwa na uwezo wa kufika mbali zaidi kwasababu bado ana nafasi ya kucheza na kufunga magoli mengi zaidi.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top