
KOCHA wa timu ya Real Madrid, Zinedine Zinade amesema mshambuliaji wa kimataifa, Cristiano Ronaldo, anastahili kupewa tuzo ya uchezaji bora wa dunia licha ya kuwa na kiwango cha kuteteleka kwa sasa
Kivutio kikubwa cha mchezaji huyo wa Ureno ni pale alipoingoza timu yake ya taifa kutwaa kombe la mataifa ya ulaya mwezi Julai.
Jitihada hizo zimekuwa zikioneka huku akiwa na nia ya kurejesha makali yake ya zamani akiwa tayari ameshapachika magoli manne kwenye mechi alizocheza.
"Anastahili kabisa kupewa Ballon D'or sio mimi binafsi ninayempigia chepuo, lakini bila shaka kila mtu anaona mwenyewe" Alisema meneja wa Real Madrid.
"Anafahamu kila kitu na anajitambua na kazi anayoifanya na ukijumuisha na watu wanaomzunguika"
Ronaldo ambaye alishatunukiwa tuzo hiyo mara tatu, ameorodheshwa kwenye list ya majina 30 wanaowania tuzo hiyo huku anayeishikilia tuzo hiyo kwa sasa naye pia akiwemo kwenye hiyo list.
Ronaldo tayari ameshacheza michezo 357 na kupachika mabao 368 huku akiwa na wastani wa kupiga bao kila mechi anayocheza.
Ingawaje alikosa mechi za awali za ligi ya Hispania pamoja na michuano ya klabu bingwa, lakini anaonekana kurejea vyema na kuendeleza historia yake.
Gme iliyopita dhidi ya Athletic club alipiga mashuti 11 sawa na jumla ya mshuti ya wapinzani wao lakini ni mawili pekee yaliyolenga goli.
"Amekuwa na hasira sana anapokuwa hashindi, na ndilo jambo jema kwa striker kama yeye" Aliongeza Zidane.
Post a Comment