
BEKI wa zamani wa timu ya Manchester United, Steve Bruce ameteuliwa kuwa kocha mkuu wa timu ya Aston Villa baada ya aliyekuwa kocha wa timu hiyo, Di Matteo kutimuliwa aliposhindwa kuiongoza timu hiyo kufanya vizuri.
Bruce aliyekuwa mkufunzi wa zamani wa Hull City alikuwa akihusishwa na kibarua cha kuinoa timu ya taifa ya England lakini dili hilo likachukuliwa na Big Sam ambaye hata hivyo hakudumu na timu hiyo.
Bruce anakuja Aston Villa akiwa na jukumu la kuhakikisha timu hiyo inarejea ligi kuu baada ya kusshuka msimu uliopita.
Post a Comment