SPORTS

 

Unknown Unknown Author
Title: KICHUYA AWASIMAMISHA MAPRO SIMBA NA YANGA.
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
HAYO ndiyo maneno ambayo tunaweza kusema baada ya Shiza Ramadhani Kichuya kuwabwaga wachezaji wa kigeni wa vilabu vikubwa kati ya Simba ...
Image result for SHIZA KICHUYA IMAGES



HAYO ndiyo maneno ambayo tunaweza kusema baada ya Shiza Ramadhani Kichuya kuwabwaga wachezaji wa kigeni wa vilabu vikubwa kati ya Simba na Yanga baada ya kuwatanguali kwa idadi ya magoli.

Hadi sasa Simba imeshacheza mechi 8 na zote Kichuya akiwa kama sehemu ya michezo hiyo na kufanikiwa kupachika magoli 6 huku akiwa kinara hadi sasa.

Kasi ya wachezaji wa kigeni kama vile Mavugo, Blagnon na hata wale wa yanga kama vile Tambwe aliyekuwa mfungaji bora msimu uliopita na Ngoma ambao ni kama bado wanasinzia.

Licha ya Kichuya ambaye ana mabao 6, Tambe tayari alishapachika magoli 4 wakati Mavugo akiwa na 3.
Image result for SHIZA KICHUYA IMAGES

Kichuya alisajiliwa kutoka klabu ya Mtibwa Sugar yenye makao yake mjini Morogoro na kuonyesha uwezo wa hali ya juu mpaka sasa.

Japo inaonekana ni kama ligi bado haijapamba moto ambapo mapro hao wanaweza kubadilika wakati wowte, lakini hadi sasa kauli ambayo inaweza kusemwa na mashabiki wengi wa mpira wa miguu ni kwamba Kichuya awakalisha mapro wa Simba na Yanga.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top