
BAADA ya kushuhudia timu ya Majimaji ikiwa na matokeo mabovu tangu msimu umeanza sasa wameonekana kuamka usingizini na kuanza kupata ushindi.
Tangu msimu huu umeanza, baada ya michezo kumi, Majimaji walikuwa wamejikusanyia jumla ya pointi 6 huku wakiwa wameshinda mechi mbili pekee.
Leo wakiwa jijini Dar es salaam, Majimaji wameibuka na ushindi wa goli 2-0 dhidi ya African Lyon na hivyo kujikusanyia jumla ya pointi 9 na kuendelea kujisogeza nafasi za juu kwenye msimamo wa ligi.
Michezo mingine iliyokuwa inapigwa leo haya hapa matokeo yake.
Ruvu Shooting 1-1 Mwadui Fc.
Ndanda FC 1-1 Mwadui FC.
Prisons 2-1 Stand United.
Toto Africa 0-2 Yanga.
African Lyon 0-2 Majimaji FC.
Post a Comment