
STAND united ambao walikuwa ni wageni kwenye uwanja wa Sokoine jijini Mbeya wamepoteza mchezo wao kwa mara ya kwanza katika msimu huu baada ya kukubali kichapo cha magoli 2-1 kutoka kwa maafande wa Jeshi la Magereza Tanzania Prisons.
Stand United walicheza mechi 10 bila kupoteza wakiwa wameshinda mechi 5 na kutoka sare mara 5 katika mechi hizo 10. Mchezo wao wa 11 wakashindwa kuendeleza rekodi yao na kuacha Simba ikiwa ndio timu pekee ambayo bado haijapoteza mchezo hadi sasa katika msimu huu wa VPL.
Licha ya kukubali kipigo hicho, bado Stand United inashika nafasi ya pili ikibaki na pointi zake zilezile 20, pointi 3 nyuma ya vinara wa ligi hiyo Simba SC.
Post a Comment