SPORTS

 

Unknown Unknown Author
Title: MAMELODI SUNDOWNS YABAKIZA DAKIKA 90 KUANDIKA HISTORIA MPYA.
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
TIMU ya Mamelodi Sundowns imejiweka mahala pazuri baada ya hapo jana kuibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya timu ya Zamalek kwenye mche...



TIMU ya Mamelodi Sundowns imejiweka mahala pazuri baada ya hapo jana kuibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya timu ya Zamalek kwenye mchezo wa fainali ya kwanza ya klabu bingwa barani Africa uliofanyia mjini Pretoria.

Shukrami kwa magoli ya Anthony Laffor, na Langerman waliopachika mabao hayo na kuiweka Sundown mguu ndani kutwaa kombe hilo.

Sundowns itakuwa ugenini wiki ijayo kusaka ushindi au sare ya aina yeyote ili kutwaa kombe hilo ikiwa ni mara yao ya kwanza na timu ya pili kutoka Africa Kusini kunyakua taji hilo baada ya kuwashuhudia Orlando Pilates wakifanya hivyo miaka iliyopita.




Wakitazamwa na mashabiki 40,000, Sundowns walikuwa na nafasi nzuri ya kuibuka na ushindi kutokana na hali ya hewa ya nchi hiyo ambapo, Sundowns waliamua kuwachezesha Zamalek jua kali.

Mchezo wa marudiano utapigwa katika dimba la Aleksandria siku ya jumapili ya tarehe 23.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top