SPORTS

 

Unknown Unknown Author
Title: KIJUSO: TUMEYAFANYIA KAZI MAKOSA YALIYOJITOKEZA DHIDI YA SIMBA.
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
KOCHA msaidizi wa timu ya Mbeya City, Mohamed Kijuso amesema makosa yaliyojitokeza kwenye mchezo wa juzi dhidi ya timu ya Simba yamesha...
dsc_1902yy



KOCHA msaidizi wa timu ya Mbeya City, Mohamed Kijuso amesema makosa yaliyojitokeza kwenye mchezo wa juzi dhidi ya timu ya Simba yameshafanyiwa kazi na timu ipo tayari kuikabiri Ruvu Shooting kwenye mchezo wa jumapili.

Akizungumza leo asubuhi kabla ya kuanza safari ya kuelekea jijini Dar es salaam kwa ajili ya mchezo huo, Kijuso alisema baada ya kupoteza mchezo dhidi ya Simba, walitumia masaa kadhaa kuangalia marudio ya mchezo huo na kubaini makosa yaliyopelekea wao kupoteza mchezo.

"Kama ulivoona tulikuwa na wakati mzuri sana kipindi cha pili, na kosa letu, tuliuanza mchezo taratibu sana, lakini tayari tunayafanyia kazi makosa yetu yote na Ruvu Shooting waitegemee Mbeya city mpya kesho kutwa" Alisema Kijuso.

Aidha, Msemaji wa klabu hiyo, Bwana Dismas Ten, alidokeza kuwa timu imeondoka na wachezaji 20 pamoja na viongozi kumi ambapo watapitiliza mpaka Dar es salaam kwa ajili ya kujiwinda na mchezo huo wa jumapili kabla ya kuwafuata Ndanda jijini Mtwara na kisha kurejea tena Dar kwa ajili ya kukipiga na African Lyon.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top