SPORTS

 

Unknown Unknown Author
Title: LUNGU AAGIZA KUAJIRIWA KWA MAKOCHA WAZAWA.
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
  RAIS wa Zambia, Edgar Lungu ameliagiza shirikisho la mpira wa miguu la nchi hiyo kuajiri makocha wazawa wa timu ya taifa ya Zambi...
 Zambia fans


RAIS wa Zambia, Edgar Lungu ameliagiza shirikisho la mpira wa miguu la nchi hiyo kuajiri makocha wazawa wa timu ya taifa ya Zambia, Chipolopolo.

 Shirikisho hilo linalofahamika kama FAZ, limekuwa likitafuta wataalamu kwa ajili ya kuwapa tenda hiyo lakini pia hata kuwa na interview na baadhi ya makocha wa kigeni.

Aliyekuwa kocha wa zamani wa timu ya taifa ya Africa Kusini, Gordon Igesund amekuwa akihusishwa na kibarua hicho baada ya kuwavutia watendaji wa shirikisho hilo kwenye mahojiano.

Lakini Lungu aliwaambia maafisa wa shirikisho hilo kwamba wasahau kuwaajiri makocha wa kigeni na badala yake wawaajiri makocha wazawa,

“Sahauni juu ya makocha wakigeni, Tunaweza kupata mafanikio na makocha wa ndani ya nchi” Alisema Lungu.

Lungu pia alitoa msaada wake kwa kocha wa muda wa Chipolopolo, Wedson Nyirenda, ambaye aliteuliwa kama mbadala wa George Lwandamina mwezi uliopita, akisema amefanya vizuri kwa muda mchache alioachiwa timu.

Hayo yamekuja baada ya Zambia kupoteza mchezo wake dhidi ya timu ya Nigeria kwa 2-1 mchezo wa kuwania kufuzu fainali za kombe la dunia za mwaka 2018, nchini Urusi.

Hata hivyo, licha ya Chipolopolo kufungwa mchezo wa kwanza, Lakini Lungu anaamini bado Zambia ina nafasi ya kufuzu fainali hizo.



About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top