SPORTS

 

Unknown Unknown Author
Title: SERGIO RAMOS KUKAA NJE MWEZI MMOJA.
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
  MLINZI wa kutumainiwa wa timu ya Real Madrid na timu ya taifa ya Hispania, aliumia kwenye mchezo wa kufuzu fainali za kombe l...


 Sergio Ramos



MLINZI wa kutumainiwa wa timu ya Real Madrid na timu ya taifa ya Hispania, aliumia kwenye mchezo wa kufuzu fainali za kombe la dunia  dhidi ya Albania, ambapo Hispania ilishinda 2-0.

Ramos 30, alitolewa nje dakika ya 80 baada ya kushindwa kuendelea na mchezo huo.

Klabu yake ya sasa Real Madrid imethibisha ya kuwa, Nahodha huyo wa Hispania amesikitishwa sana na jeraha hilo la goti litakalomweka nje kwa zaidi ya majuma manne.

Aidha, imeripotiwa kuwa, Ramosi atakuwa nje kwa takribani mwezi mmoja ambapo ataikosa baadhi ya mechi za ligi ukiwemo ule wa mahasimu wao Atletico Madrid. 

Lakini pia Ramos ataukosa mtanange wa ligi ya mabingwa dhidi ya Legia Warsaw na akiwa mashakani kucheza mechi dhidi ya Macedonia ya kufuzu fainali za kombe la dunia tarehe 12 ya November.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top