
OLIVIER Giroud bado haelewi sababu hasa ya
kwanini baadhi ya mashabiki wa Ufaransa ambao ni vipenzi wa Karim Benzema
ambaye ameenguliwa kwenye timu hiyo walichagua kumzomea wakati wa Michuano ya
Euro mwaka huu.
Mshambuliaji
huyo wa Arsenal aliifungia Ufaransa mabao matatu kuelekea hatua ya fainali, huku
Benzema akiwa hayupo kwenye kikosi hicho kutokana na kuwa katika uchunguzi juu
ya sakata lake la picha za utupu na mchezaji mwenza Mathieu Valbuena
Sauti
kutoka baadhi ya sehemu za uwanjani zilisikika zikimzomea Giroud hali ambayo
haikuwa ikimfurahisha kutokana na kuamini kutostahili kufanyiwa vitendo hivyo.
“Nilikuja
kugundua kwamba watu waliokuwa wakinizomea hawakuwa wale wasio nipenda bali ni
wale ambao wanampenda Benzema,” alisema.
“Sijui
kwanini waliamua kufanya vile. Niltoka kwenye ligi nikiwa na msimu mzuri kabisa
na Arsenal. Kiukweli sikujisikia vizuri kwa walichokifanya.”
Giroud
alifunga goli moja katika ushindi wa mabao 3-1 kwenye mchezo wa kirafiki dhidi
ya Italy..
Mpaka
sasa amefunga mabao 21 kwenye michezo 56 aliyocheza kwenye taifa hilo.
Post a Comment