SPORTS

 

Unknown Unknown Author
Title: UFUNGUZI WA KOZI YA UKOCHA KWA WANAWAKE.
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
picha na Boiplus. KOZI ya ukocha kwa wanawake ngazi ya FIFA imefunguliwa rasmi leo kwa ajili ya kufundisha makocha wanawake itakayofany...
picha na Boiplus.

KOZI ya ukocha kwa wanawake ngazi ya FIFA imefunguliwa rasmi leo kwa ajili ya kufundisha makocha wanawake itakayofanyika kwa siku tano.

Kozi hiyo itakayofanyika katika ukumbi wa mikutano wa TFF imefunguliwa na moja ya wajumbe wa Baraza la Michezo la Taifa, Bi. Jennifer Mmasi.

Kozi hiyo itatolewa na mkufunzi toka FIFA Bi Andrea Ronebaugh na makocha wanaotarajia kujifunza kozi hiyo ni 26 toka mikoa mbalimbali ya Tanzania kwa ajili ya kulikuza soka la wanawake nchini.

Kozi hiyo inakuja siku chache kabla ya kuanza kwa ligi ya soka la wanawake itakayoanza mwezi ujao.

Aidha mwenyekiti wa soka la wanawake Bi Amina Ngaula amewataka makocha hao pindi wamalizapo kozi hiyo wasikae nyumbani bali watumie uwezo wao kwa ajili ya kukuza soka la wanawake nchini.

Nae mkufunzi wa kozi hiyo Bi Andrea amelipongeza shirikisho la mpira wa miguu nchini kwa kukubali kozi hiyo ifanyike hapa nchini.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top